OnlineApp
eRITA Portal

Country | Category |
|---|---|
Tanzania | Government |
> ABOUT SERVICE (KUHUSU HUDUMA):
RITA ni wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini Tanzania kwa ajili ya usajili wa kielekroniki wa kuzaliwa, vifo, ndoa, talaka na usajili wa wadhamini.
> INSTRUCTIONS (MAELEKEZO):
MAOMBI MAPYA YA USAJILI WA VIZAZI:
Mambo muhimu ya kuzingatia unapofanya maombi:
Tunza taarifa ulizotumia kufungua akaunti,
Mwombaji awe na taarifa zake sahihi pamoja na wazazi wote wawili,
Mwombaji atapata Ankara ya malipo na atatakiwa kulipa kwa njia ya Benki (NMB and CRDB) au Mitandao ya simu (M-PESA, TIGO PESA and AIRTEL Money) tu kwa mujibu wa maelezo utakayopewa.
Mwombaji awe na nakala laini (soft copies) za viambatanisho vinavyotakiwa katika mfumo wa pdf,
Mwombaji aainishe wilaya atakayochukulia cheti
Aidha, Tunapenda kuwasisitizia waombaji wote kufuata maelekezo hapo juu ili kuepuka usumbufu. Anuani ya maombi ya eRITA pamoja na Mwongozo wa maombi ya huduma yanapatikana hapo chini ya ukurasa huu Kumbuka: maombi hayatafanyiwa kazi kabla ya kukamilisha malipo ya ada ya huduma. Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0800 117 482
CHETI CHA KUZALIWA CHA ZAMANI KWENDA KIPYA:
Huduma hii ni kwa wale waliopata cheti cha kuzaliwa kisichokuwa kwenye mfumo wa kielektroniki, hivyo wanasajili kupitia huduma hii ili wapate cheti cha kielektroniki.
MAOMBI MAPYA YA USAJILI WA VIFOMAOMBI MAPYA YA USAJILI WA VIFO:
Mambo muhimu ya kuzingatia unapofanya maombi:
Tunza taarifa ulizotumia kufungua akaunti,
Mwombaji awe na taarifa zake sahihi pamoja na wazazi wote wawili,
Mwombaji atapata Ankara ya malipo na atatakiwa kulipa kwa njia ya Benki (NMB and CRDB) au Mitandao ya simu (M-PESA, TIGO PESA and AIRTEL Money) tu kwa mujibu wa maelezo utakayopewa.
Mwombaji awe na nakala laini (soft copies) za viambatanisho vinavyotakiwa katika mfumo wa pdf,
Mwombaji aainishe wilaya atakayochukulia cheti
Aidha, Tunapenda kuwasisitizia waombaji wote kufuata maelekezo hapo juu ili kuepuka usumbufu. Anuani ya maombi ya eRITA pamoja na Mwongozo wa maombi ya huduma yanapatikana hapo chini ya ukurasa huu Kumbuka: maombi hayatafanyiwa kazi kabla ya kukamilisha malipo ya ada ya huduma.
CHETI CHA KIFO CHA ZAMANI KWENDA KIPYA:
Huduma hii ni kwa wale waliopata cheti cha kifo kisichokuwa kwenye mfumo wa kielektroniki, hivyo wanasajili kupitia huduma hii ili wapate cheti cha kielektroniki.
UHAKIKI WA VYETI VYA VIZAZI NA VIFO:
Hii ni huduma mpya inayomuwezesha muombaji kuwasilisha maombi ya kuhakiki cheti cha kuzaliwa na kifo kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote. Muombaji atatakiwa kuscan cheti cha kuzaliwa au kifo anachohitaji kihakikiwe na kisha kukituma kwa njia ya kieletroniki ili kihakikiwe. Majibu ya uhakiki yatatumwa katika akaunti uliyofungua sehemu iliyoandikwa "DETAILS" na utapakua cheti ulichotuma kwa ajili ya uhakiki.