top of page

OnlineApp

NIDA Online Services

OnlineApps.png
Country
Category
Tanzania
Government

> ABOUT SERVICE (KUHUSU HUDUMA):

NIDA ni mamlaka ya vitambulisho vya taifa Tanzania, kuna aina tatu za vitambulisho,

1. Uraia (hutolewa kwa raia mwenye umri kuanzia miaka 18 na zaidi)

2. Mgeni mkazi (hutolewa kwa mgeni mkazi anayeishi nchini kihalali kuanzia miezi 6 na kuendelea)

3. Mkimbizi (hutolewa kwa mkimbizi mwenye hati ya ukimbizi)

Huduma tajwa hapo juu zinahusisha usajili, marekebisho wa taarifa za usajili na kuhuisha kitambulisho cha taifa kwa aliyepoteza na kupata kingine.

> INSTRUCTIONS (MAELEKEZO):

Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa ujazaji fomu mtandaoni:

  1. Mwombaji anatakiwa kuwa na anuani ya barua pepe ambayo ataitumia kujisajili na kupokea kiunga kitakachomuwezesha kukamilisha usajili wake.
  2. Mwombaji anatakiwa kuwa na nyaraka zisizopungua mbili zitakazotumika kuthibitisha utambulisho wake. Mfano wa nyaraka hizo ni; Cheti cha kuzaliwa n.k.
  3. Mwombaji anatakiwa kufanya “scanning” ya nyaraka zake na kuziweka katika muundo wa PDF (usiozidi kurasa moja kwa kila kiambatisho) au picha katika muundo wa JPG au PNG.
  4. Ni muhimu Mwombaji kujaza Namba yake ya simu ya mkononi.
  5. Mwombaji anatakiwa kuambatisha cheti cha kuzaliwa endapo amezaliwa Mwaka 1980 na kuendelea. Aidha, endapo Mwombaji amezaliwa kabla ya mwaka 1980 anatakiwa kuambatisha cheti cha kuzaliwa au “Affidavit”.
  6. Kwa Waombaji wenye majina mengine; ni vyema kuandika majina hayo ili endapo ikatokea uhitaji wa kurekebisha majina yake iwe rahisi kutambulika.
  7. Mwombaji anatakiwa kufahamu majina ya Baba na Mama yake mzazi.
  8. Mwombaji ambaye ana Namba za Utambulisho (NIN) za wazazi wake; anatakiwa kuweka viambata halisi (kwa wazazi waliokwishapata vitambulisho vya Taifa).
  9. Mwombaji anatakiwa kujua namba ya Nyumba, Mtaa na kata anayoishi.

10. Kwa Watanzania walioko nje ya Nchi, wanatakiwa kupata uthibitisho wa ukaazi katika Nchi husika kutoka kwa Afisa wa Ubalozi wa Tanzania ili kujaza sehemu ya makazi, Mtaa/Kata kwa usahihi.

11. Endapo Mwombaji amepata vyeti vya Shule, Namba ya mlipa kodi (TIN) na Kadi ya mpiga kura; ni vyema kuambatanisha.

12. Mwombaji anatakiwa kujaza Fomu kwa usahihi na kuhakikisha viambata vyake na taarifa alizo jaza katika mfumo hazikinzani na taarifa nyingine, kama vile taarifa za Shule au Biashara.

13. Mwombaji anatakiwa kujaza taarifa zake kwa usahihi, na kuchapisha taarifa hizo katika fomu na kwenda kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa napoishi kwa ajili ya kugongewa Mhuri na Saini ya Mwenyekiti wa Mtaa wake.

14. Mwombaji anatakiwa kufika katika Ofisi ya NIDA iliyoko kwenye Wilaya yake ya makazi akiwa na fomu iliyokamilika (Fomu iliyogongwa Mhuri na kuwekwa Saini ya Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa), pamoja na nakala ngumu za viambatisho vyake alivyopakia katika mfumo wakati wa usajili kwa ajili ya kukamilisha taratibu za usajili.

15. Kwa Mwombaji ambaye anahitaji kupata maelezo ya ziada; asisite kufika katika ofisi ya NIDA iliyopo karibu.

Jinsi ya kujaza fomu ya Usajili kwa raia kwa mkono:-

Jaza fomu ya maombi ya Utambulisho wa Taifa Namba 1A kwa kalamu ya wino mweusi na kwa herufi kubwa. (Fomu inapatikana kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA, Wilayani/Serikali ya Mtaa na kwenye tovuti yetu)

fomu ya maombi ya Utambulisho wa Taifa Namba 1A

Hakikisha una saini fomu yako ya maombi ya Utambulisho wa Taifa kwenye kipengele Namba 59/60 ama umeweka alama ya dole gumba iwapo hauna saini rasmi ama hujui kusoma na kuandika,

Gonga muhuri fomu yako ya Maombi ya Utambulisho wa Taifa kwenye Serikali ya Mtaa unakoishi kipengele namba 59/60 na kuandikiwa barua ya utambulisho wa makazi,

Ambatisha nyaraka zifuatazo, viambatisho hivi ni vya lazima:
    i.   Cheti cha kuzaliwa,
    ii.  Barua ya utambulisho wa makazi kutoka Serikali ya Mtaa unakoishi,
    iii. Cheti cha kuzaliwa au Kitambulisho cha Taifa cha mzazi mmoja.

Ambatisha viambatisho vya ziada ulivyonavyo kati ya vifuatavyo:
    i.  Vyeti vya Masomo-Msingi,Sekondari,Chuo,
    ii.  Pasi ya kusafiria,
    iii. Leseni ya udereva,
    iv. Namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN),
    v.  Kadi ya bima ya afya,
    vi. Kitambulisho cha mzanzibar mkaazi

Wasilisha fomu yako ya maombi kwenye Ofisi ya Usajili ya NIDA wilaya unakoishi kwa ajili ya kuchukuliwa alama za kibaiolojia (kupigwa picha, kuweka saini ya kielektroniki na kuchukuliwa alama za vidole) ili kupisha hatua zinazofuata ziendelee.

Mavazi ya kuzingatia wakati wa Usajili: Ili picha ya mwombaji wa Utambulisho wa Taifa itoke katika ubora uliokusudiwa pindi unapowasilisha fomu ya maombi kwenye ubalozi husika kupigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole, unashauriwa kutovaa nguo; nyeupe, kijivu, bluu mpauko, pinki au nguo za kung’aa, jezi, nguo zenye nembo, michoro au maandishi, kofia aina yoyote na kutopaka hina viganjani ili alama za vidole zisomeke kirahisi,

Hatua mbalimbali za usajili na utambuzi wa watu:-
    i.  Ujazaji wa fomu za Utambuzi na Usajili,
    ii. Uhakiki wa awali wa fomu za maombi,
    iii. Uingizaji wa taarifa kwenye mfumo wa kompyuta,
    iv. Kuthibitishaji taarifa za mwombaji zilizo katika mfumo wa kompyuta,
    v.  Uchukuaji wa alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki,
    vi. Utengenezaji wa Daftari Kuu la Taarifa za Watu,
    vii. Uhakiki wa mwisho,
    viii.Uchapishaji, uhakiki wa ubora na Utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.

Ufafanuzi wa mambo msingi hitajika kwa baadhi ya hatua za usajili tajwa hapo juu;

1.1.1. Usajili – Ujazaji wa fomu (biographic data)

Mwombaji wa Kitambulisho Raia, Mgeni ama Mkimbizi anatakiwa kufika katika kituo/ofisi ya usajili na vivuli (Copy) ya nyaraka za kutambulisha makazi, uraia na umri wake kama ilivyoainishwa hapo juu katika kipengele cha mahitaji ya kila kundi wakati wa usajili.

1.1.2. Uchukuaji alama za kibaiolojia

Hatua hii ya Usajili inajumuisha upitiaji wa taarifa za mwombaji katika mfumo, uchukuliwaji wa alama za vidole, picha na utiaji wa saini ya kielektroniki ambapo kuna mambo msingi ya mwombaji kuzingatia ambayo ni;

Kwa ajili ya ubora na mwonekano mzuri wa picha mwombaji unashauriwa kutovaa nguo nyeupe, pinki, kijivu, bluu mpauko au nguo zenye rangi za kungaa sana. Kutovaa kofia ya aina yoyote wakati wa kupiga picha, au kupaka hina viganjani wakati wa uchukuaji wa alama za kibaiolojia.

Ili kurahisisha zoezi hili, mwombaji unaombwa kufika kwenye ofisi/kituo cha usajili na nyaraka halisi (original) za kuthibitisha uraia na umri wake mathalani, cheti cha kuzaliwa, pasipoti, vyeti vya elimu ya msingi na sekondari, leseni ya udereva, kitambulisho cha bima ya afya, kitambulisho cha mpigakura na kitambulisho cha mzanzibar mkazi.

1.1.3. Uhakiki na Uwekaji Pingamizi

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika hatua hii inakuwa ikiendesha zoezi la kupokea maoni ya uwekaji pingamizi kutoka kwa wananchi juu ya wakazi waliofanya maombi ya kupatiwa Vitambulisho vya Taifa na Uhakiki wa mwisho wa taarifa za waombaji kabla ya kuanza uchapaji na ugawaji wa Vitambulisho kwa wakazi ambao wamekamilisha hatua ya kuchukuliwa alama za kibaiolojia (picha, alama za vidole na saini ya kielektroniki).

NIDA kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za Mitaa, vyombo vya usalama na wananchi kwa jumla inakuwa ikipokea taarifa za maoni au pingamizi kuhusiana na waombaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa wakazi wa maeneo husika. Hii ni hatua muhimu katika kutekeleza azma ya Serikali ya kujenga mfumo madhubuti wenye taarifa na kumbukumbu sahihi za watu, hivyo wananchi wanaweza kutoa pingamizi la kimaandishi wakieleza sababu ya pingamizi kwa kuainisha upungufu ambao wamebaini, mathalani taarifa za URAIA, UMRI, MAJINA, PICHA na MAKAZI ya mwombaji kwa kujaza fomu maalum kwenye mtaa husika au kutoa taarifa NIDA kwa kutuandikia barua kupitia anuani S.L.P 12324 Dar es Salaam, barua pepe, au kuziwasilisha kwenye Ofisi za wilaya husika.

NIDA inawaomba wananchi kuwa wazalendo na kujitokeza kuhakiki taarifa zao na waombaji wengine, na kutoa pingamizi bila upendeleo, uonevu au kukomoana.

1.1.4. Ugawaji Vitambulisho vya Taifa

Mwombaji anatakiwa kufika katika ofisi ya usajili katika wilaya husika ama kulingana na maelekezo/matangazo yanayotolewa katika eneo hilo ili kupatiwa kitambulisho chake kwa kuzingatia kuja na risiti maalumu aliyopatiwa na NIDA wakati alipokamilisha kuchukuliwa alama za kibaiolojia.

USAJILI NA UTAMBUZI WA MGENI MKAAZI:

Wageni Wakaazi wenye umri wa miaka 18 na zaidi wanaoishi nchini Tanzania kulingana na hati ya ukaazi wanaarifiwa kujitokeza Kusajiliwa kwa mujibu wa sheria ya Usajili na Utambuzi wa watu kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA wilayani.

Unapofika kwenye ofisi ya Usajili wilayani tafadhali wasilisha nyaraka zifuatazo:

1.Pasi ya kusafiria ya nchi unakotoka,

2. Hati ya kibali cha kazi,

3.Hati ya kibali cha ukaazi (nakala mbili (2)),

4.Ankara ya malipo ya benki (bank pay slip) kulingana na daraja la kundi la mgeni husika kama ilivyoainishwa hapo chini:-
    i.Mgeni $ 100,
    ii.Mfanyakazi $ 50,
    iii.Mmisionari, Mtafiti, na Mwanafunzi, $ 20,
    iv. Mtegemezi $ 20.

Malipo yote yafanyike kupitia akaunti ya NIDA ya benki ya NMB/CRDB/NBC au PBZ baada ya kupatiwa Namba ya Malipo ya Huduma za Serikali (Controll Number) kwenye ofisi ya Usajili wilayani ama kielektroniki kupitia kiunganishi

Malipo yakishafanyika hayarudishwi. Unashauriwa kuwasiliana na Ofisi ya Usajili husika kabla ya kufanya malipo ili kuepuka usumbufu usio wa lazima

Jinsi ya kujaza fomu ya Usajili kwa Mgeni Mkaazi:-

1. Jaza fomu ya maombi ya Utambulisho wa Taifa Namba 2A kwa kalamu ya wino mweusi na kwa herufi kubwa. (Fomu inapatikana kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA, Wilayani/Serikali ya Mtaa na kwenye tovuti yetu - www.nida.go.tz au kwa kufungua

fomu ya maombi ya Utambulisho wa Taifa Namba 2A

2. Hakikisha una saini fomu yako ya maombi ya Utambulisho wa Taifa kwenye kipengele Namba 42 ama umeweka alama ya dole gumba iwapo hauna saini rasmi ama hujui kusoma na kuandika,

3. Gonga muhuri fomu yako ya Maombi ya Utambulisho wa Taifa kwenye Serikali ya Mtaa unakoishi kipengele namba 43 na kuandikiwa barua ya utambulisho wa makazi,

4. Wasilisha fomu yako ya maombi kwenye Ofisi ya Usajili ya NIDA wilaya unakoishi kwa ajili ya kuchukuliwa alama za kibaiolojia (kupigwa picha, kuweka saini ya kielektroniki na kuchukuliwa alama za vidole) ili kupisha hatua zinazofuata ziendelee.

5. Mavazi ya kuzingatia wakati wa Usajili: Ili picha ya mwombaji wa Utambulisho wa Taifa itoke katika ubora uliokusudiwa pindi unapowasilisha fomu ya maombi ofisi ya Usajili ya NIDA wilayani kupigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole, unashauriwa kutovaa nguo; nyeupe, kijivu, bluu mpauko, pinki au nguo za kung’aa, jezi, nguo zenye nembo, michoro au maandishi, kofia aina yoyote na kutopaka hina viganjani ili alama za vidole zisomeke kirahisi

Hatua mbalimbali za usajili na utambuzi wa watu:-
    i.  Ujazaji wa fomu za Utambuzi na Usajili,
    ii. Uhakiki wa awali wa fomu za maombi,
    iii. Uingizaji wa taarifa kwenye mfumo wa kompyuta,
    iv. Kuthibitishaji taarifa za mwombaji zilizo katika mfumo wa kompyuta,
    v.  Uchukuaji wa alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki,
    vi. Utengenezaji wa Daftari Kuu la Taarifa za Watu,
    vii. Uhakiki wa mwisho,
    viii.Uchapishaji, uhakiki wa ubora na Utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.

Ufafanuzi wa mambo msingi hitajika kwa baadhi ya hatua za usajili tajwa hapo juu;

1.1.1. Usajili – Ujazaji wa fomu (biographic data)

Mwombaji wa Kitambulisho Raia, Mgeni ama Mkimbizi anatakiwa kufika katika kituo/ofisi ya usajili na vivuli (Copy) ya nyaraka za kutambulisha makazi, uraia na umri wake kama ilivyoainishwa hapo juu katika kipengele cha mahitaji ya kila kundi wakati wa usajili.

1.1.2. Uchukuaji alama za kibaiolojia

Hatua hii ya Usajili inajumuisha upitiaji wa taarifa za mwombaji katika mfumo, uchukuliwaji wa alama za vidole, picha na utiaji wa saini ya kielektroniki ambapo kuna mambo msingi ya mwombaji kuzingatia ambayo ni;

Kwa ajili ya ubora na mwonekano mzuri wa picha mwombaji unashauriwa kutovaa nguo nyeupe, pinki, kijivu, bluu mpauko au nguo zenye rangi za kungaa sana. Kutovaa kofia ya aina yoyote wakati wa kupiga picha, au kupaka hina viganjani wakati wa uchukuaji wa alama za kibaiolojia.

Ili kurahisisha zoezi hili, mwombaji unaombwa kufika kwenye ofisi/kituo cha usajili na nyaraka halisi (original) za kuthibitisha uraia na umri wake mathalani, cheti cha kuzaliwa, pasipoti, vyeti vya elimu ya msingi na sekondari, leseni ya udereva, kitambulisho cha bima ya afya, kitambulisho cha mpigakura na kitambulisho cha mzanzibar mkazi.

1.1.3. Uhakiki na Uwekaji Pingamizi

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika hatua hii inakuwa ikiendesha zoezi la kupokea maoni ya uwekaji pingamizi kutoka kwa wananchi juu ya wakazi waliofanya maombi ya kupatiwa Vitambulisho vya Taifa na Uhakiki wa mwisho wa taarifa za waombaji kabla ya kuanza uchapaji na ugawaji wa Vitambulisho kwa wakazi ambao wamekamilisha hatua ya kuchukuliwa alama za kibaiolojia (picha, alama za vidole na saini ya kielektroniki).

NIDA kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za Mitaa, vyombo vya usalama na wananchi kwa jumla inakuwa ikipokea taarifa za maoni au pingamizi kuhusiana na waombaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa wakazi wa maeneo husika. Hii ni hatua muhimu katika kutekeleza azma ya Serikali ya kujenga mfumo madhubuti wenye taarifa na kumbukumbu sahihi za watu, hivyo wananchi wanaweza kutoa pingamizi la kimaandishi wakieleza sababu ya pingamizi kwa kuainisha upungufu ambao wamebaini, mathalani taarifa za URAIA, UMRI, MAJINA, PICHA na MAKAZI ya mwombaji kwa kujaza fomu maalum kwenye mtaa husika au kutoa taarifa NIDA kwa kutuandikia barua kupitia anuani S.L.P 12324 Dar es Salaam, barua pepe, au kuziwasilisha kwenye Ofisi za wilaya husika.

NIDA inawaomba wananchi kuwa wazalendo na kujitokeza kuhakiki taarifa zao na waombaji wengine, na kutoa pingamizi bila upendeleo, uonevu au kukomoana.

1.1.4. Ugawaji Vitambulisho vya Taifa

Mwombaji anatakiwa kufika katika ofisi ya usajili katika wilaya husika ama kulingana na maelekezo/matangazo yanayotolewa katika eneo hilo ili kupatiwa kitambulisho chake kwa kuzingatia kuja na risiti maalumu aliyopatiwa na NIDA wakati alipokamilisha kuchukuliwa alama za kibaiolojia.

Sifa Stahiki kwa Mwombaji Mwenye Hitaji la Kuboresha Taarifa za Usajili: -

(i)Mwombaji aliyeolewa na kubadilisha jina kwa kutumia taarifa za ukoo wa mume/mwenza wake,

(ii) Mwombaji aliyeolewa na kuachika kisheria anaweza kuruhusiwa kubadilisha taarifa zake na kurudia kujiandikisha kwa majina yake ya awali ya kabla hajaolewa kulingana na vyeti/nyaraka zake

(iii) Mwombaji aliyekosea kuandika baadhi ya taarifa zake yeye mwenyewe ambazo aliziandikisha wakati wa zoezi la Usajili na Utambuzi.

(iv) Mwombaji ambaye taarifa zake hazikuingizwa kwa usahihi kwenye mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa na Watendaji wake wakati wa utekelezaji wa majukumu husika (Operational issues),

(v) Mwombaji ambaye aliandikisha taarifa/majina yake yoyote kwenye kipengele cha majina mengine/maarufu na baadaye akahitaji majina yake hayo yaandikwe kwenye kipengele cha majina ya kwanza basi ataweza kurekebishiwa bila kuathiri utambulisho wake wa awali au taarifa zilizohifadhiwa katika mfumo.

(vi) Jina la ukoo iwapo mwombaji ataamua kutumia jina ambalo tayari lipo kwenye upande wa majina ya wazazi wake mfano jina la Babu ambalo hapo awali hakulitumia.

Afisa Usajili wa Wilaya (DRO) anaweza akaridhia kubadilisha taarifa ambazo ziko kwenye fomu ya maombi ya Mwombaji ambazo ziliandikishwa hapo awali mfano katika sehemu ya majina mengineyo na iwapo mabadiliko hayo hayana nia ovu au yenye lengo la kuficha Utambulisho wake wa awali.

Taarifa za Maombi ya Utambulisho wa Watu zinazoruhusiwa kubadilishwa

Mwongozo wa marekebisho ya Taarifa za Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa unaelekeza juu ya taarifa zinazoruhusiwa kubadilishwa iwapo m waombaji kakidhi vigezo vya msingi vinavyo hitajika ni pamoja na; -

(i)Jina la kwanza, la kati, au la Mwisho (Ukoo) baada ya kukidhi vigezo na kuwasilisha uthibitisho unaotakiwa,

(ii)Tarehe na mwezi wa kuzaliwa,

(iii)Makazi ya mwombaji,

(iv)Namba ya simu baada ya Afisa Usajili kujiridhisha ya kwamba Namba ya Simu imesajiliwa kwa kutumia NIN ya Mwombaji.

(v)Uraia kwa yule aliyebadilisha uraia kwa nyaraka zinazokubalika kwa kufuata mwongozo wa Uhuishaji wa Taarifa za Uraia

(vi)Taarifa ya ndoa,

(vii)Taarifa ya kazi pamoja na

(viii)Kumbukumbu binafsi (taarifa hizi zinapatikana kwenye kipengele F cha fomu ya Usajili na Utambuzi wa Watu Na. 47- 58.)

Taarifa za Mwombaji zisizoruhusiwa kubadilishwa isipokuwa kwa kibali maalumu baada ya kufanyiwa kazi na Kamati ya Usajili na Utambuzi na kupata idhini ya Mkurugenzi Mkuu

(i)Taarifa za Wazazi

(ii)Makazi ya Kudumu

(iii)Mahali pa kuzaliwa

(iv)Majina mawili/ matatu

(v)Mwaka wa kuzaliwa na

(vi)Saini ya mwombaji

KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA "NEED HELP" HAPO CHINI

bottom of page