top of page

OnlineApp

TRC SGR Ticketing Online

OnlineApps.png
Country
Category
Tanzania
Public Sector

> ABOUT SERVICE (KUHUSU HUDUMA):

SGR Tanzania ni reli ya kisasa na ya kwanza Africa mashariki na kati itakayokuwa na uwezo wa kupitisha treni zitakazoendeshwa kwa nishati ya umeme na yenye mwendo kasi usiopungua kilometa 160 kwa saa.

Lengo la reli hii ni kuongeza ufanisi katika sekta ya usafirishaji nchini ususani sekta ya reli ambapo yafuatayo yatarahisishwa;

  • Ongezeko la usafirishaji wa mizigo ambapo reli itabeba mzigo wa mpaka tani 10,000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa maroli 500 ya mizigo.
  • Uokoaji wa muda kwa usafiri wa abiria na mizigo ambapo itasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
  • Ongezeko la ajira kwa wazawa katika sekta na fani mbalimbali.
  • Oboreshaji wa huduma za kijamii ikihusisha ujenzi wa shule, vituo vya afya na ujenzi wa barabara katika maeneo yanayo pitiwa na mradi.
  • Kuchochea maendeleo katika secta ya kilimo, biashara, madini na viwanda hususani katika maeneo ambapo reli hiyo inapita pamoja na kwa nchi jirani hasa Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na DRC.
  • Faida za kiuchumi kwenye sekta ya usafirishaji hasa kupunguza gharama za mara kwa mara za matengenezo ya barabara.

> INSTRUCTIONS (MAELEKEZO):

Zingatia haya wakati wa ukataji wa tiketi:

  • Kitambulisho cha uraia (kama ni mtanzania)
  • Hati ya kusafiria
  • Cheti cha kuzaliwa kwa mtoto

 

bottom of page